Ashtakiwa ICC kwa uharibifu wa maeneo ya kihistoria

Haki miliki ya picha AP
Image caption Makavazi ya Timbuktu baada ya kurekebishwa

Mwanamgambo mmoja wa kiislamu anayeshukiwa kuharibu maeneo ya kihistoria na kitamaduni katika mji wa Timbuktu nchini Mali, amepelekwa katika mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC kukabaliana na mashtaka yanayohusu uhalifu wa kivita

Ahmad Al Mahdi Al Faqi alikabidhiwa mahakama hiyo kutoka utawala wa Niger

Waendesha mashtaka wanasema kuwa alihusika katika kuharibu maeneo ya kihistoria mwaka 2012 wakati Timbuktu ilipokuwa chini ya udhibiti kwa makundi ya wanamgambo.

Hii ndiyo kesi ya kwanza inayohusu uharibifu wa maeneo ya kihistoria kufikishwa mbele ya mahakama ya kimataifa ya ICC.