Ufaransa yashambulia IS Syria

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ufaransa yashambulia IS Syria

Ufaransa imekuwa taifa la hivi punde zaidi kuanzisha mashambulizi ya angani dhidi ya wapiganaji wa kiislamu wa Islamic State nchini Syria.

Afisi ya rais imetangaz kuwa wametekeleza mashambulizi hayo usiku wa kuamkia leo baada ya kukusanya ujasusi katika majuma mawili yaliyopita.

Jeshi la Ufaransa limekuwa likitekeleza mashambulizi dhidi ya kundi hilo nchini Iraq kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Australia pia imekuwa ikiishambulia Islamic State

Wakati huo huo Wakuu wa kijeshi wa Iraq, wanasema kuwa wanajishughulisha na taarifa ya ujasusi na operesheni ya usalama kwa ushirikiano na Urusi, Iran na Syria, ili kukabiliana na tahadhari kutoka kwa kundi la wanamgambo wa kiislamu wa Islamic State.

Wairaqi wanasema kuwa wamekuwa wakifuatilia madai kuhusiana na ongezeko la watu wenye itikadi kali, wanaosafiri kutoka Moscow Nchini Urusi na kufika katika maeneo

Haki miliki ya picha IS
Image caption Ufaransa yashambulia IS Syria

hayo kwa nia ya kushiriki katika mapigano.

Ni dalili za hivi punde za Urusi kuhusika katika maswala ya mashariki ya kiti hasa nchini Syria ambapo imetuma vikosi vyake vingi vya kijeshi hatua ambayo imeibua tumbo joto huko Washington.