Mwaka 1 tangu wanafunzi 43 kutoweka Mexico

Haki miliki ya picha nc
Image caption Maelfu ya watu wamejitokeza kuishinikiza serikali kutoa ukweli kuhusu vifo vya wanafunzi 43

Mwaka mmoja uliopita, wanafunzi 43 walipotea katika mji wa Iguala katika jimbo la Guerrero, kusini mwa Mexican.

Maelfu ya watu wanashiriki katika maandamano makubwa katika mji mkuu wa Mexico kuadhimisho mwaka mmoja tangu kutokea kwa kisa hicho.

Uchunguzi wa serikali ulidai kuwa, wanafunzi hao walikabidhiwa kwa genge moja la uhalifu, ambao waliwauwa na kisha kuteketezwa mabaki ya maiti yao katika eneo la urushwaji taka.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Mwaka 1 tangu wanafunzi 43 kutoweka Mexico

Ripoti hiyo haijakataliwa tu na jamaa ya wanafunzi hao, bali pia ripoti kutoka kwa kundi moja la wataalamu wa uchunguzi huru, hivi majuzi ilihoji uhalali wa ripoti hiyo ya uchunguzi wa serikali.

Bernardo Santos Campos, babake Hose Angel, Ameiambia BBC kuwa wazazi wa wanafunzi hao waliotoweka hawatasitisha maandamano kamwe, hadi watakapojua kilichofanyika.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Kesi hiyo ni nembo ya kutoweka kwa maelfu ya raia wa Mexico

Rais wa Mexico Enrique Pena Nieto, ameahidi uchunguzi upya ufanywe.

Kesi hiyo ni nembo ya kutoweka kwa maelfu ya raia wa Mexico, ambao wametoweka katika muongo mmoja wa ghasia inayohusisha makundi hasimu ya ulanguzi wa dawa za kulevya na walinda usalama.