Kundi la Taliban lashambulia Kunduz

Haki miliki ya picha
Image caption Mwanajeshi wa Afghanistan huko Kunduz

Mamia ya wapiganaji wa kundi la Taliban wametekeleza mashambulizi katika mji wa Kunduz uliopo kaskazini mwa Afghanistan.

Wapiganaji wanatekeleza mashambulizi hayo kutoka pembe tofauti na wameripotiwa kuingia katika hospitali moja kwa mda.

Kuna majeruhi kutoka pande zote kulingana na maafisa wa polisi.

Mkoa wa Kunduz umeshuhudia idadi kadhaa ya mashambulizi tangu mwezi Aprili ,huku Taleban likishirikiana na wapiganaji wengine.

Mashambulio hayo yanaijri siku moja baada shambulizi la bomu katika mechi moja mashariki mwa mkoa wa Paktika kuwaua watu tisa.

Shambulizi hilo la siku ya jumatatu mjini Kunduz linaonekana kuwa muhimu kwa kundi la Taliban.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Wapiganaji wa Aghanistan wakijitayarisha kukabiliana na wanamgambo wa Taleban

Kundi la Taliban linasema kuwa limeingia katika hospitali ya Kunduz,lakini vyombo vya habari vimesema kuwa lilikaa tu kwa mda.

Picha katika mitandao ya kijamii zimeonyesha wapiganaji hao wakijipiga selfi ndani ya hospitali hiyo.

Msemaji wa polisi katika mkoa wa Kunduz Sayed Sarwar Hussaini aliliambia shirika la habari la Reuters kwamba ,vita vikali vingali vinaendelea katika maeneo ya Khanabad,Chardara pamoja na Imam Sahed,ikiwa ndio njia kuu inayoingia katika mji huo.

''Tuna vikosi vya kutosha na tutawafurusha''.

Amesema kuwa wapiganaji 20 wamefariki katika vita hivyo,huku ikiwa haijulikani ni wanajeshi wangapi wa serikali waliouawa.