Ng’ombe wawekwa ‘reflector’ Zimbabwe

Ng'ombe Zimbabwe
Image caption Wakazi wanasema kamba hizo zitawawezesha madereva kuwaona mifugo hao kutoka mbali

Wakazi wa wilaya moja nchini Zimbabwe wamevumbua njia ya kuzuia ajali za barabarani zinazohusisha ng’ombe wanaoranda randa.

Wamekuwa wakiwaweka kamba au vitambaa vinavyoakisi mwanga shingoni au kwenye mikia.

Wakazi hao wa wilaya ya Gutu, mkoa wa Masvingo wanasema hilo litakuwa likiwawezesha waendeshaji magari kuwatambua ng’ombe hao kutoka mbali.

Ng’ombe wengi walitoweka kwenye mashamba baada ya Wazungu wengi kufurushwa kutoka kwa mashamba yao mwaka 2000 kufuatia agizo la Rais Mugabe. Wengi wao wamekuwa wakizurura zurura bila wa kuwatunza. Mashamba mengi pia yalibaki bila ua.