Ghasia zaidi zazuka al-Aqsa Jerusalem

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ghasia al-Aqsa

Kumetokea ghasia zaidi kati ya vikosi vya usalama vya Israel na raia wa Palestina kandokando ya msikiti mkubwa wa Al Aqsa mjini Jerusalem.

Maafisa wa polisi wawalirushia vitoa machozi vijana waliokuwa wakirusha mawe na mabomu ya petroli.

Eneo hilo lililopo katika maeneo yanayokaliwa na wayahudi na waislamu ni eneo takatifu.

Haki miliki ya picha
Image caption Ghasia al Aqsa

Ni eneo la mizozo mara kwa mara lakini wasiwasi umeongezeka katika majuma ya hivi karibuni.

Hii ni kwa sababu raia wa Palestina wanashuku kwamba Israel inataka kubadilisha usimamizi wa eneo hilo swala linalopingwa na Israel.