Wanamuziki wakamatwa Somaliland

Image caption Wanamuziki wa Somaliland wanaruhusiwa kutumbuiza popote ulimwenguni isipokuwa Somalia

Wanamuziki maarufu wa Somaliland, the Horn Stars, wamekamatwa wakituhumiwa kupunga bendera ya Somalia kwenye Tamasha.

Kundi hilo lilikuwa likitumbuiza katika sikukuu ya Eid al-Adha mjini Mogadishu nchini Somalia.

Wanamuziki wanne wanatuhumiwa kutumbuiza kwa nyimbo zinazopinga uhuru wa Somaliland.

Somaliland ilijitangazia uhuru wake kutoka Somalia mwaka 1991 lakini haijatambuliwa kimataifa.

Wanamuziki hao walikamatwa wakati waliporejea Somaliland katika mji mkuu wa nchi hiyo, Hargeisa siku ya jumapili.

Katika mtandao wa Twitter watu wameanza kutoa maoni yao wakitaka wanamuziki hao kuachiwa huru.

Naibu waziri wa mambo ya ndani wa Somali land Ahmed Adarre amesema ''Wasanii wanaweza kutumbuiza popote duniani lakini sio Somalia.hivyo hawapaswi kujihusiaha na siasa'' alieleza.