Mwezi usio wa kawaida waibua msisimko

Mwezi mkubwa Haki miliki ya picha EPA
Image caption Picha hii inaonyesha mwezi mkubwa wa kawaida na mwezi mkubwa ukilingana na kupatwa kwa mwezi kama ilivyoshuhudiwa Wiesbaden, Ujerumani leo

Watu wengi pande mbalimbali duniani wamekuwa wakitazama tukio la kawaida la kupatwa kwa mwezi ambalo limetokea wakati mmoja na kuonekana kwa mwezi mkubwa kwa Kiingereza "supermoon".

Mwezi huo mkubwa huonekana mwezi unapokuwa karibu zaidi na njia ya mzunguko ya dunia, jambo ambalo huufanya kuonekana mkubwa angani.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mwezi mkubwa ulivyoshuhudiwa angani London

Kupatwa kamili kwa mwezi – ambako huufanya kuwa na rangi nyekundu – kulionekana Amerika Kaskazini, Afrika Magharibi na Ulaya Magharibi.

Image caption Mwezi mkubwa usio wa kawaida unavyotokea

Tukio hili lilitokea mara ya mwisho 1982 na mara nyingine litaonekana 2033.