Ajali:Ng'ombe wavishwa vimuliko Zimbabwe

Image caption Ngombe wavalishwa vimuliko Zimbabwe

Wakaazi wa wilaya moja iliopo mashambani nchini Zimbabwe wamezindua njia itakayosaidia kupunguza ajali za ng'ombe wanapovuka barabara.

Raia hao wameamua kuwawekea vimuliko katika mikia na shingo.

Wakaazi wa Gutu mkoani Masvingo wanasema kuwa vimuliko hivyo vya rangi ya manjano vitawaonya madereva kuhusu wanyama hao wanozurura.

Wanasema kuwa wengi walitoroka kufuatia kufurushwa kwa wamiliki wa mashamba mwaka 2000 wakati ambapo baadhi ya ua ziliharibiwa