Madaktari wapata idhini ya kupandikiza tumbo la Uzazi

Haki miliki ya picha AP
Image caption Madaktari nchini Uingereza wamepata idhini ya kupandikiza tumbo la uzazi la wanawake kwa mara ya kwanza.

Madaktari nchini Uingereza wamepata idhini ya kupandikiza tumbo la uzazi la wanawake kwa mara ya kwanza.

Katika majaribio hayo ya kimatibabu, madaktari hao watapandikiza nyumba ya mtoto kwa wanawake kumi katika hatua ya kwanza.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mtoto wa kwanza kuzaliwa baada ya mamake kupandikizwa tumbo la uzazi

Mwaka jana mtoto mmoja nchini Sweden, alikuwa mtu wa kwanza duniani kuzaliwa kupitia uhamisho wa kizazi kwa mamake.

Kinyume na wenzao wa Sweden, kikosi hicho cha madaktari kutoka Uingereza, kitatatumia viungo kutoka kwa wafadhili wa jamaa ya waliofariki.

Haki miliki ya picha Other
Image caption Madaktari kutoka Uingereza, watatatumia viungo kutoka kwa wafadhili wa jamaa ya waliofariki

Madaktari hao wamefanya kazi hiyo kwa zaidi ya miaka 20 ili kupata idhini ya majiribio hayo.

Ziadi ya wanawake mia moja tayari wametambuliwa kwa nia ya kufanyiwa majaribio hayo.