Mwanariadha wa Sierra Leone hataishi Uingereza

Image caption Mkimbiaji Jimmy Thoronka wa Sierra Leone akosa kibali cha kuishi Uingereza

Mkimbiaji Raia wa Sierra Leone aliyetoweka baada ya kushiriki michuano ya jumuia ya madola huko Glasgow na kisha kujitokeza baadae kuomba kibali cha kuishi Uingereza amekataliwa ombi lake.

Jimmy Thoronka, hakurejea nyumbani baada ya mashindano hayo msimu wa joto mwaka 2014, kutokana na hofu ya maradhi ya Ebola nchini mwake.

Thoronka alikamatwa baada ya kuonekana kulala hovyo mitaani , lakini alipatiwa ufadhili wa masomo na Chuo kikuu cha London.

Msemaji wa Wizara ya mambo ya ndani amethibitisha kukataliwa kwa ombi la mkimbiaji huyo kwa kuwa hakutimiza masharti ya sheria za uhamiaji.

Takriban watu 4000 walipoteza maisha kutokana na mlipuko wa maradhi ya Ebola.

Wazazi wa Thoronka pia walipoteza maisha kutokana na virusi vya ugonjwa huo.

Akitambuliwa kuwa mwanariadha maarufu nchini hakupata Medali yeyote kwenye michuano hiyo.