Kundi la Taliban lafurushwa Kunduz

Haki miliki ya picha
Image caption Jeshi la Afghanistan

Maafisa wa Afghanistan wanasema kuwa wamedhibiti maeneo muhimu ya mji wa kaskazini wa Kunduz kutoka kwa wapiganaji wa Taliban.

Oparesheni iliotekelezwa usiku kucha imesababisha kuchukuliwa kwa maeneo muhimu ya serikali mbali na kusababisha uharibifu mkubwa kwa wapiganaji.

Lakini wapiganaji wa Taliban wanasisitiza kuwa wanashikilia maeneo makubwa ya mji huo.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Jeshi la Afghanistan

Kutekwa kwa mji huo siku ya jumatatu na kundi hilo la wapiganaji ilikuwa pigo kubwa kwa rasi Ashraf Ghani,wakati ambapo alikuwa anasherehekea mwaka mmoja tangu achukue mmlaka.

Iwapo itathibitishwa,utakuwa ushindi mkubwa kwa jeshi la Afghanistan,ikiwa ni jaribio kubwa la kijeshi tangu kuonolewa kwa vikosi vya muungano mnamo mwezi Disemba mwaka uliopita.