Mbunge kuadhibiwa kwa kusifu serikali ya ubaguzi wa rangi

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mandela na aliyekuwa kiongozi wa serikali ya Afrika kusini FW De Clerk

Chama rasmi cha upinzani nchini Afrika Kusini kimeanzisha hatua za kinidhamu dhidi ya mbunge mmoja mwandamizi,ambaye alionekana akimsifu mwanasiasa mmoja wa nyakati za ubaguzi wa rangi.

Diane Kohler Barnard wa muungano wa kidemokrasia ameomba msamaha kwa kusambaza ujumbe wa facebook uliosema kwamba hali ya afya,elimu na huduma za polisi zilikuwa zimeimarika wakati wa ubaguzi wa rangi chini ya uongozi wa P.W. Botha.

Chama hicho kimetaja maoni yake kama yasio na utetezi.kumekuwa na wito wa kumtaka ajiuzulu.

Muungano wa kidemokrasia,ambao ulimchagua kiongozi wa kwanza mweusi miezi minne iliopita unajaribu kujenga uaminifu miongoni mwa raia wengi wa Afrika kusini walio weusi.