Daktari 'bandia' ashtakiwa Kenya

Image caption Mugo wa Wairimu

Raia mmoja wa Kenya ameshtakiwa na makosa 12 ikiwemo ubakaji,kujifanya kuwa mkunga mbali na kufungua kliniki bila leseni jijini Nairobi.

Mugo wa Wairimu amakana mashataka hayo na awali alikuwa oia amekana kwamba alim'baka mgonjwa wake baada ya kumpatia dawa za kulala.

Mashtaka hayo ni pamoja na kanda ya video iliorushwa hewani na runinga moja nchini Kenya iliokuwa ikimuonyesha mtu asiyejulikana akimnyanyasa kingono mwanamke asiye na fahamu katika kitanda cha kliniki hiyo.

Muungano wa madaktari nchini Kenya umesema kuwa daktari huyo ni bandia.