Ni haramu kutoa peremende badala ya chenji Kenya

Image caption Notisi iliotolewa na benki kuu Kenya.

Benki kuu ya Kenya imetoa taarifa katika magazeti ya leo nchini humo ikiyataka maduka kusita kutoa vitu mbadala vya masalio ya sarafu ya taifa hilo.

Baadhi ya maduka yamekuwa yakitoa mda wa maongezi ya simu,viberiti na hata peremende badala ya kutoa masalio yanayohitajika kulingana na mwandishi wa BBC Joseph Odhiambo.

Image caption Sarafu

Lakini benki kuu imesema kuwa kuna ina sarafu za kutosha na kuziagiza benki zote nchini kuhakikisha kuwa sarafu hizo zinasambazwa.