Wafanyakazi wa MSF wauawa Kunduz

Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Wafanyakazi wa MSF wauawa Kunduz

Shirika la madaktari wasio na mipaka la Medecins Sans Frontieres, linasema watatu kati ya wafanyi kazi wake wameuawa na wengine 30 hawajulikani waliko baada ya zahanati yao kushambuliwa katika mji wa Kunduz nchini Afghanistan.

Kulingana na shirika hilo zahanati hiyo iliharibiwa vibaya na mabomu.

Haki miliki ya picha MSF
Image caption Wafanyakazi wa MSF wauawa Kunduz

Shirika la kujihami la nchi za magharibi NATO linasema kuwa linachunguza kubaini ikiwa shambulizi la marekani lilihusika.

Kumekuwa na mapigano makali katika mji wa Kunduz tangu wapiganaji wa Taliban kuuvamia siku ya Jumatatu.