Machar atofautiana na Kiir kuhusu majimbo

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Machar na kiir

Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir, ameongeza idadi ya majimbo ya nchi hiyo, kutoka 10 hadi kufikia 28.

Msemaji wake alieleza kuwa hatua hiyo itaimarisha huduma, na kuwapa madaraka zaidi watu.

Kiongozi wa wapiganaji, Riek Machar, alisema Bwana Kiir amekwenda kinyume na makubaliano ya amani yaliyotiwa saini mwezi uliopita, ambayo msingi wake ni nchi kuwa na majimbo 10.

Makubaliano hayo yalitarajiwa kumaliza vita vya karibu miaka miwili, lakini mapambano yameendelea.