Kanisa Katoliki linajadili upya familia

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Papa Francis amewaomba makasisi hao wawe na moyo wa kupokea mabadiliko katika maisha ya waumini wa kanisa hilo.

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani papa Francis anaongoza misa katika makao makuu ya Vatican wakati wa kuanza kwa wiki tatu za mkutano wa maaskofu wa kikatoliki kuhusu mabadiliko ya mifumo ya maisha.

Inatarajiwa kuwa mkutano huo utafichua tofuati kati ya viongozi dhabiti wa kikatoliki na wale wanaopendelea utamaduni kwa upande mmoja huku wengine wenye misimamo wastani wanaokubali mabadiliko ya sera yanayoendelea kanisani kama vile ndoa za wapenzi wa jinsia moja na pia talaka ama hata watoto waliozaliwa nje ya ndoa.

Mwandishi wa BBC aliyeko huko anasema kuwa kanisa hilo huenda lisibadilishe mifumo yake kuhusu masuala ya familia licha ya watunza tamaduni kudai kuwa kanisa hilo linaonekana kuchanganyikiwa na sera kanisa katoliki.

Image caption Papa Francis akiwapokea wapenzi wa jinsia moja

Hi majuzi tu kiongozi mmoja wa kidini alitimuliwa kazini baada ya kubainika kuwa alikuwa katika uhusiano wa mapenzi ya jinsia moja.

Papa Francis amewaomba makasisi hao wawe na moyo wa kupokea mabadiliko katika maisha ya waumini wa kanisa hilo.