12 wauawa kwenye mafuriko Ufaransa

Image caption 12 wauawa kwenye mafuriko Ufaransa

Takriban watu 12 wameaga dunia kusini mwa ufaransa baada ya mvua iliyoandamana na upepo mkali kusababisha mafuriko eneo hilo.

Watu watatu waliuawa katika nyumba moja ya watu wazee karibu na eneo la Antibes huku mmoja akizama maji katika mji wa Cannes.

Watabiri wa hali ya hewa wanasema kuwa zaidi ya mililita 175 za mvua zilinyesha ndani ya saa mbili siku ya Jumamosi usiku.