Wapalestina wazuiwa kuingia Jerusalem

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wapalestina wazuiwa kuinga Jerusalem

Polisi wa Israeli wametangaza marufuku ya kuingia kwenye mji wa kale wa Jerusalem hatua ambayo itasababisa wapalestina kutoruhusiwa eneo hilo kwa siku mbili.

Hii ni baada ya mashambulizi yaliyofanyika dhidi ya raia wa Israeli siku ya Jumamosi na Jumapili asubuhi.

Wawili hao waliuawa kwa kuchomwa kisu na mpalestina, huku kijana mmoja naye akijeruhiwa katika kisa tofauti.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu anafanya mkutano wa dharura na baraza la mawaziri

Polisi waliwaua kwa kuwapiga risasi washambuliaji hao.

Wapalestina hawaruhusiwi kuingia eneo hilo isipokuwa wale wanaoishi huko.

Hata hivyo waisraeli na wamiliki wa biashara pamoja na wanafunzi pekee ndio watakaoruhusiwa kuingia.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Utawala wa Palestina umekashifu hatua ya Israeli ya kupalia cheche za uhasama

Waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu anafanya mkutano wa dharura na baraza la mawaziri kujadili matukio hayo.

Utawala wa Palestina umekashifu hatua ya Israeli ya kupalia cheche za uhasama katika ukingo wa Magharibi na Jerusalem katika kipindi cha hivi punde.