MSF yataka uchunguzi huru Kunduz

Haki miliki ya picha MSF
Image caption Hospitali mjini Kunduz iliyolipuliwa kwa mabomu

Shirika la madaktari wasio na mipaka mjini Kunduz Kaskazini mwa Afghanistan wametaka uchunguzi huru ufanywe kubaini aliyerusha mabomu katika hospitali yao huku wakiwa wanawalaumu wanajeshi wa Marekani.

Shirika hilo limesema shambulio ambalo liliua wafanyakazi kumi na wawili na kujeruhi wengine kumi ni uhalifu wa kivita na halitaweza kuchunguzwa na Wamarekani.

Katibu mkuu wa jeshi la marekani Ash Carter, ameahidi kuwa na uwazi katika uchunguzi ingawa kuna mazingira yanayochanganya na kutatanisha.

Madaktari hao wasio na mipaka wamekataa madai ya Marekani kuwa mapigano hayo ya anga yalikuwa yame walenga wapiganaji wa Talban ambao walikuwa karibu na hospitali.

Wamesisitiza kuwa mashambulizi yalikuwa si sahihi kwani yalijirudia rudia.Hata hivyo huduma hizo za kujitolea zimesimamishwa mjini Kunduz.