Mercedes yazindua lori linalojiendesha

Image caption Mercedes yazindua lori linalojiendesha

Amini usiamini huku watu wengi Afrika Mashariki wakilazimika kulipa mabilioni ya shilingi ilikujifunza kuendesha magari,teknolojia sasa imepiga hatua moja zaidi.

Mwanzo ilikuwa ni magari madogo sasa kampuni ya kutengeneza magari ya kifahari Daimler Mercedes-Benz imezindua lori linalojiendesha lenyewe!

Mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo yenye asili yake nchini Ujerumani,Wolfgang Bernhard alibofya kidude na mara lori likachukua usukani na kuenda lenyewe pasi na kusababisha ajali ya aina yeyote.

Haki miliki ya picha Daimler
Image caption Lorry hilo aina ya Actross lilijaribiwa katika barabara inayotumika na uma ya Baden-Wurttemberg Ujerumani.

Lori hilo linatumia teknolojia ya kamera kwa pamoja na 'radar' kukwepa magari mengine barabarani.

Aidha mtambo huo unatuma na kupokea taarifa na mawasiliano iwapo lori hilo linasogea karibu zaidi kitu chochote iwe ni gari,mti ama hata mtu barabarani.

Hata hivyo kampuni hiyo ilisisitiza kuwa sharti dereva awe hapo wakati wote kifaa hicho cha "highway pilot" kinapotumika kama tahadhari kusitokee ajali.

Haki miliki ya picha Daimler
Image caption Hata hivyo kampuni hiyo ilisisitiza kuwa sharti dereva awe hapo wakati wote kifaa hicho cha "highway pilot" kinapotumika kama tahadhari kusitokee ajali.

Lorry hilo aina ya Actross lilijaribiwa katika barabara inayotumika na uma ya Baden-Wurttemberg Ujerumani.

Kwa mujibu wa bwana Bernhard lori hilo lilimudu kujiendesha na hata kutimia kasi ya Kilomita 80 kwa saa.

Haki miliki ya picha Daimler
Image caption Mfumo huo unatumia miale kubaini kona na maelezo kwenye mabango barabarani.

Mkurugenzi huyo alikuwa na Waziri Winfried Kretschmann walikuwemo ndani ya lori hilo wakati wa jaribio hilo la kihistoria.

Bernhard alissistiza kuwa wakati dereva anapohisi amechoka gari hilo linaweza kuchukua usukani naye ajipumzishe kidogo japo kwa kutengeneza kikombe cha chai huku kamera na mfumo huo wa radar zikidhibiti usukani.

Haki miliki ya picha Daimler
Image caption Bernhard alissistiza kuwa wakati dereva anapohisi amechoka gari hilo linaweza kuchukua usukani naye ajipumzishe kidogo

Mfumo huo unatumia miale kubaini kona na maelezo kwenye mabango barabarani.

''Kwa hakika hata uwe mstadi kivipi , mfumo huu wa "highway pilot" unaendesha vyema zaidi kuliko mwanadamu na hata iwe kwa kiwango kipi haiwezi kuchoka sawa na vile madereva wa malori huwa wanawachoka na kupoteza umakinifu barabarani.'' alisema mkurugenzi wa kampuni hiyo Wolfgang Bernhard.