Albino waliokatwa mikono TZ wapata msaada

'Uovu ambao umeliaibisha taifa'.

Image caption Pendo, ambaye ana miaka 15 alishambuliwa mwezi Agosti

Hivyo ndivyo rais wa Tanzania Jakaya mrisho Kikwete ameelezea mauaji ya albino wapatao 80 tangu mwaka 2000 nchini Tanzania.

Image caption Baraka ambaye anafikisha miaka sita baadaye mwezi huu alishambuliwa mnamo mwezi Machi.

Wengine wengi wamekatwa viungo mbalimbali vya mwili kwa kuwa wengi wanaamini kwamba viungo vyao vinaleta bahati nzuri.

Image caption Emmanuel, mwenye umri wa miaka 13, anaweza kutumia mkono wake mpya kufanya kazi za kawaida

Lakini kundi moja la watoto waliopoteza mikono katika shambulizi wamepewa fursa mpya.

Image caption Mkono wake wa bandia sasa unamsaidia kupika

Walisafiri hadi nchini Marekani ili kuwekewa mikono bandia.Wanne kati ya watano sasa wamerudi nchini Tanzania.