Je,ni kweli mitandao inapunguza mahaba?

Image caption Wapenzi

Mwana historia na mwanahabari mmoja wa runinga Lucy Worsley amesema kuwa mahaba yanaendelea kupotea miongoni mwa wanadamu kwa kuwa imekuwa rahisi kukutana na watu wapya kupitia programu za kuwakutanisha wapenzi pamoja na mtandao.

katika mahojiano na Redio Times amesema kuwa wapendanao hawapitii vikwazo ambavyo vilisababisha mahaba kukithiri katika siku za nyuma.

Lakini wataalam wa uhusiano wa kimapenzi wanasema kuwa sio watu wote walio na uwezo wa kujitolea.

Kuna watu kadhaa ambao huona vigumu kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na hulazimika kukimbilia washauri.

Haki miliki ya picha Ayush
Image caption Mtandao wa Tinder

Wengi hutumia mtandao wa Tinder.

Ijapokuwa mtandao huo hautoa nambari za wateja wake,unasema kuwa watu hukutanishwa mara milioni 26 kila siku huku Huku mtandao huo ukiwa umewakutanisha watu bilioni 8 uzinduliwe mwaka 2012.

Utafiti wa hivi majuzi umebaini kwamba huku vijana wadogo wakiwa wamekutana na wapenzi wao kupitia programu za kuwakutanisha na wapenzi wao au mitandao,kwa juma,wengi wa watu 6000 waliohojiwa wanasema kuwa walikutana na wapenzi wao katika hali ya ana kwa ana.