NATO yainyooshea kidole Urusi

Haki miliki ya picha RIA
Image caption Ndege za kijeshi za Urusi

NATO imeituhumu Urusi baada ya ndege zake za kivita kuruka mara mbili isivyo sahihi katika anga ya Uturuki.

Muungano huo ulisema kuwa ni lazima Moscow kuachana na suala hilo na kuelezea kwa nini ilifanya ukiukwaji huo.Pia ilitoa wito kwa Urusi kuacha mashambulizi yake dhidi ya upinzani nchini Syria pamoja na raia na kulenga zaidi kupigana dhidi ya wapiganaji wa kiislam wa IS.

Mapema Uturuki ilipinga matumizi ya nguvu dhidi ya ndege za jeshi za Urusi.(Urusi inafanya mashambulizi mazito ya ya mabomu kwa lengo la kumuunga mkono Rais Assad wa Syria ambapo Uturuki imeelezea kuwa ni kosa kubwa.