Wanafunzi 20 washtakiwa na ulevi Kenya

Image caption Mahakama

Zaidi ya wanafunzi 70 leo wamefikishwa mahakamani mjini Eldoreti nchini Kenya baada ya kukamatwa katika ukumbi wa densi wa chini ya ardhi wakiwa na pombe , miraa, bangi na mipira ya kondomu.

Awali wanafunzi 500 walikamatwa katika uvamizi uliofanywa Jumapili jioni, lakini wengi waliachiliwa kwa sababu walikua na umri mdogo.

Wanafunzi hao walikua katika hafla ya kurejea shule maarufu kama ''back to school party'' kusherehekea kikomo cha mgomo wa waalimu wa wiki tano nchini humo.