Wafanyakazi Korea Kusini ‘walipia’ usingizi

Kulala Haki miliki ya picha Getty
Image caption Wafanyakazi Seoul sasa wamekuwa hawalali kwenye viti afisini

Wafanyakazi wanaohudumu katika afisi nyingi mji mkuu wa Korea Kusini, Seoul wamekuwa wakilipa kupata usingizi wakati wa maakuli ya mchana.

Wamekuwa wakitembelea vyumba maalum vya kulala na kupumzika “kumaliza uchovu”.

Kwa mujibu wa gazeti la Chosun Ilbo, vyumba hivyo vimekuwa maarufu sana hasa maeneo ya jiji yenye afisi nyingi.

Vyumba hivyo vya starehe ambavyo hujaa sana wakati wa maankuli huwapa watu fursa ya kulala, na vingine vina hata viti vya kukandia misuli.

Mmoja wa wanaotembelea vyumba hivyo alinukuliwa na Chosun Ilbo akisema: "Nilizoea kulala kwenye kiti kazini au kujifungia chooni, lakini sasa ninaweza kulala chini hapa na kupata usingizi kwa starehe.”

Raia wa Korea Kusini hufanya kazi saa nyingi Zaidi miongoni mwa mataifa yaliyoendelea, na wengi hufadhaika kutokana na kazi.

Utafiti uliofanywa na Shirikisho la Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo uligundua raia wa Korea Kusini hufanya kazi saa 2,163 kwa mwaka ukilinganisha na saa 1,388 nchini Ujerumani.