Volkswagen kurekebisha magari yake

Haki miliki ya picha
Image caption Mkurugenzi mpya kampuni ya Volkswagen Matthias Mueller

Kampuni ya magari ya Volkswagen imesema magari yake yaliyoathirika na sakata ya gesi chafu yatafanyiwa marekebisho.

Mkurugenzi mpya wa kampuni hiyo ya magari, Matthias Mueller amesema magari hayo yanatarajiwa kurudishwa ili kufanyiwa marekebisho kuanzia mwaka ujao.

Ameliambia gazeti moja nchini ujerumani kuwa mengi ya magari millioni 11 yanayotumia mafuta ya dizeli yatafanyiwa marekebisha madogo ya mitambo.