Jurgen Klopp apewa kandarasi Liverpool

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Jurgen Klopp

Jurgen Klopp amekubali kandarasi ya miaka mitatu kuwa mkufunzi wa kilabu ya Liverpool.

Raia huyo wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 48 anachukua mahala pake Brendan Rodgers ambaye alifutwa kazi siku ya jumapili baada ya kuiongoza timu hiyo ambayo iko nafasi ya 10 katika jedwali la ligi ya Uingereza kwa miaka mitatu na nusu.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Brendan Rodgers

Klopp hajakuwa akifunzi timu yoyote tangu mwezi Mei,wakati alipomaliza ukufunzi wake wa miaka saba katika klabu ya Borussia Dortmund ili kuchukua likizo.

Anatarajiwa kumleta Zeljko Buvac na Peter Krawietz,manaibu wake wa zamani katika kilabu hiyo ya Bundesliga ili kujaza safu yake ya ukufunzi.