Kesi dhidi ya wanajeshi 11 wa Rwanda zafutwa

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Jenerali Karake Karenzi

Mahakama ya juu nchini Uhispania imefutilia mbali kesi dhidi ya wanajeshi 11 kati ya 40 walioshtakiwa mwaka 2008 kwa mashtaka yaliodaiwa kutekelezwa baada ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda mwaka 1994,kulingana na wakili anayewakilisha baadhi ya waathiriwa.

Jordi Palou aliimbia BBC kwamba ni wale wasiokabiliwa na mashtaka ya ugaidi ambao kesi zao zimefutiliwa mbali.

Watu hao ni pamoja na Jacques Nziza,ambaye wachanganuzi wanasema ni wa pili kwa uwezo mkubwa baada ya rais wa Rwanda Paul Kagame.

Mashtaka hatahivyo yataendelea dhidi ya watu wengine 29 waliosalia,akiwemo mpelelezi mkuu wa Rwanda Karenzi karake na waziri wa ulinzi jenerali James Kabarebe.

Bwana Palou anasema kuwa kesi zao zinasubiri na kwamba maagizo ya kuwakamata huenda yakatekelezwa.

Jenerali Karake alikamatwa nchini Uingereza mamo mwezi Juni kupitia agizo lililotolewa na Uhispania,lakini ombi la kumsafirisha lilikataliwa.

Waziri wa haki nchini Rwanda Johnstone Busingye amesema kuwa serikali imekuwa ikisema kuwa kesi hizo dhidi ya wanajeshi ni za uongo,zenye msukumo wa kisiasa na na unyanyasaji wa haki zao kulinga na gazeti la New Times linalounga mkono serikali ya Rwanda.