Pembe za ndovu: Raia wa Uchina wakamatwa TZ

Image caption Uwindaji haramu

Jopo maalum la wanyama pori nchini Tanzania limewakamata baadhi ya raia wa Uchina wanaoshukiwa kusafirisha pembe za ndovu.

Makundi ya kampeni dhidi ya uwindaji haramu yanasema kuwa wale waliokamatwa ni pamoja na mwanamke aliyepewa jina la utani 'Malkia wa pembe za ndovu' Yang Feng Glan.

Wahifadhi wameitaja Tanzania kama shina la uwindaji haramu wa pembe za ndovu, na kuongezea kuwa ndovu 8,500 waliuawa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita.