Wasifu wa bi Anna Mghirwa

Image caption Wasifu wa bi Anna Mghirwa

Anna Mghirwa ni mwenyekiti wa Chama cha Alliance for Change and Transparency Tanzania, ACT wazalendo.

Yeye mgombea pekee wa kike wa kinyang'anyiro cha urais mwaka 2015

Alizaliwa tarehe 23 mwezi Januari mwaka 1959.

Alijiunga na chama cha ACT mwezi Machi mwaka huu akitokea Chadema licha ya kuwa Chama kichanga, kilichoundwa mwaka jana.

Mama Anna si mgeni katika ulingo wa siasa.

Alikuwa mwanachama wa TANU Tanganyika African National Union kabla ya kuundwa kwa CCM,akiwa mwanachama wa umoja wa vijana na hata kushinda tuzo mbalimbali kutokana na ushiriki wa juu katika chama cha Tanu.

Hata hivyo baada ya ku undwa kwa Chama cha CCM alipunguza ushiriki wake kwa sababu za kifamilia na masomo.

Amesomea theologia na ni mkufunzi wa sheria .

Kwa kipindi kirefu,Hakuwa akijihusisha na siasa hadi alipoamua kujiunga na chama cha CHADEMA mwaka 2009 baada ya kukamilisha mpango wake wa masomo.

Katika Chama cha ChAdema alishika nafasi za uenyekeiti wa baraza la wanawake ngazi ya wilaya na baraza la wanawake mkoa.

Image caption Alizaliwa tarehe 23 mwezi Januari mwaka 1959.

Mwezi Machi mwaka huu alijiunga na rasmi na ACT Wazalendo na katika Mkutano Mkuu wa kwanza wa chama hicho, alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa kwanza wa ACT.

Mwanamama huyu si mashuhuri lakini uthubutu wake wa kuwa mwanamke pekee katika kinyang'anyiro cha Urais mwaka huu kumemfanya awe maarufu

Hata hivyo wachambuzi wa mambo wanaona kuwa mwanamama huyu ni mgeni kwenye ulingo wa siasa hajajipambanua vya kutosha hivyo kukomaa na kuwa na uwezo wa kiasi cha kupata wadhifa mkubwa kwenye jamii.

Mwenyewe anasema ana uzoefu wa kutosha katika maswala ya uongozi na hata ameshafanya kazi za maendeleo kwa muda mrefu katika uendeshaji wa serikali za mitaa pia katika mashirika ya kitaifa na kimataifa akijihusisha na maswala ya wanawake, watoto,na pia maswala ya harakati.

Kinachomsukuma mama Anna Mghirwa katika kuwatumikia Watanzania ni ile dhamira yake ya kutaka kuhakikisha kuwa Wanawake wanakuwa sehemu ya kuleta maendeleo..

Amefanya kazi mbalimbali za kitaaluma, amekuwa mwalimu wa vyuo vikuu Tanzania na msimamizi wa miradi mbalimbali ya kitaifa na nje ya nchi

Mghirwa alijitosa ubunge kwa mara ya kwanza mwaka 2012 baada ya Tume ya taifa ya uchaguzi kutangaza uchaguzi mdogo katika jimbo la Arumeru Mashariki, kaskazini mwa Tanzania baada ya kifo cha Mbunge Solomon Sumari.

Image caption Mama Anna amewafungulia mlango wanawake wengine kupata motisha kugombea nNafasi za Juu hasa za katika siasa.

Pia amewahi kugombea ubunge wa bunge la Afrika mashariki, kupitia Chadema japokuwa hakufanyikiwa.

Pamoja na uzoefu katika kulitumikia taifa na hata jumuia ya kimataifa, yeye ni mwanamke wa kawaida sana.

Mama wa watoto watatu ni mwanamke mwenye kujichanganya na wengine na kusaidia wasiojiweza.

Licha ya baadhi wachambuzi wa siasa kuelezea kuwa huenda asifanikiwe kuwa rais wanakubaliana kuwa mama Anna amewafungulia mlango wanawake wengine kupata motisha kugombea nNafasi za Juu hasa za katika siasa.