Blatter aenda mahakamani

Image caption Blatter akata rufaa dhidi ya uamuzi

Rais wa FIFA Sepp Blatter amekata rufaa dhidi ya uamuzi wa kamati ya maadili ya FIFA wa kumsimamisha kazi kwa siku tisini .

Raia huyo wa Uswizi mwenye umri wa miaka 90 amepigwa marufuku kushiriki katika kazi zozote huku kamati ya maadili ya FIFA ikichunguza madai ya ufisadi dhidi ya viongozi wa FIFA.

Alisimamishwa kazi siku ya Alhamisi pamoja na katibu wake Jerome Valcke na makamu wa rais Michel Platini.

Platini amesema kuwa atapinga uamuzi huo katika njia na wakati unaofaa.

Wote watatu wamekana kufanya uovu.