Mafuriko yakumba mji mkuu wa Ghana

Image caption Mafuriko Ghana

Mafuriko yamerudi tena katika mji mkuu wa Ghana ,Accra baada ya saa mbili za mvua kubwa mapema siku ya Ijumaa kulingana na mwandishi wa BBC Sammy Darko.

Image caption Mafuriko Ghana

Mara ya mwisho kwa mji huo kukumbwa na mafuriko ilikuwa mwezi Juni,wakati ambapo moto katika kituo kimoja cha mafuta ya petroli ambapo watu wengi walikuwa wamejikinga mvua ulisababisha vifo vya watu 100.