Mitambo ya umeme kufungwa Tanzania

Image caption Gazeti la The Citizen nchini Tanzania

Gazeti la the Citizen nchini Tanzania limeripoti kwamba mitambo ya kuzalisha umeme kwa kutumia maji itafungwa kutokana na viwango vya chini vya maji.

Gazeti hilo limemnukuu waziri wa kawi George Simbachawene akisema kuwa baadhi ya mabwawa yanakaribia kukauka.

''Tangu tulipopata uhuru,hatujapungukiwa na maji na kufikia viwango tunavyoviona leo.Lazima tufanye uamuzi huu mgumu wa kuzima vituo hivyo vya umeme''.