Kijana aliyewadunga kisu Waisraeli auawa

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Israeli

Polisi wa Israeli wanasema kuwa kijana Mpalestina amewadunga kisu Waisraeli wawili mjini Jerusalem.

Polisi walimpiga risasi na kumuua kijana huyo.Madaktari wanasema kuwa wawili hao wako katika hali nzuri.

Hicho ndicho kisa cha hivi punde cha raia wa Israeli kudungwa kisu na kusababisha hali tete katika eneo hilo.

Polisi pia wanasema kuwa mwanamme mmoja Mpalestina amepigwa risasi na kujeruhiwa vibaya wakati wa makabiliano kusini mwa mji wa Jerusalem.

Polisi wanasema kuwa mwanamme huyo alipigwa risasi baada ya kuwafyatulia risasi polisi wa kulinda mpaka nchini Israeli katika kambi ya wakimbizi ya Shuafat.