Bieber ataka picha zake za uchi kuondolewa mtandaoni

Haki miliki ya picha PA
Image caption Msanii Justin Bieber

Mawakili wa msanii wa muziki wa Pop Justin Bieber wanataka picha zote za utupu za msanii huyo kuondolewa katika mitandao mara moja.

Mwandishi wa Hollywood amedai kwamba ameona barua iliotumwa kwa mtandao wa New York News,ambao ulichapisha picha za nyota huyo wa muziki akiwa katika likizo huko Polynesia Ufaransa.

Piacha hizo zilizopigwa Bora Bora bado zipo katika mtandao huo.

Barua hiyo inataka hatua kuchulkuliwa katika saa 12 baada ya kupata agizo hilo.

Barua hiyo imethibitisha kuwa picha hizo ni za Bieber ,licha ya uvumi kwamba huenda zimekarabatiwa ili kufanana na msanii huyo.