Wanajeshi wa Uganda bado wapo S Kusini

Wanajeshi wa Uganda katika kikosi cha Umoja wa Afrika Haki miliki ya picha

Uganda inasema wanajeshi wake bado wangaliko Sudan Kusini ingawa wakati uliowekwa kwa wao kuondoshwa umepita.

Wanajeshi wote wa kigeni wanatakiwa wawe wamehamishwa Jumamosi ikiwa ni sharti muhimu katika makubaliano ya amani yaliyotiwa saini karibuni baina ya serikali ya Sudan Kusini na wapiganaji.

Wanajeshi wa Uganda walitumwa Sudan Kusini miaka miwili iliyopita kufuatana na ombi la Rais Salva Kiir.

Msemaji wa jeshi la Uganda, Luteni Kanali Paddy Ankunda, alisema hakujatolewa amri kwa wanajeshi hao kuondoka.

Mahala pao panatarajiwa kuchukuliwa na kikosi cha nchi jirani ambacho bado hakiko tayari.