Prasad Oli ndiye waziri mpya wa Nepal

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Prasad Oli ndiye waziri mpya wa Nepal

Bunge la Nepal limemchagua waziri mkuu mpya, Khadga Prasad Oli, huku nchi ikkabiliwa na upungufu mkubwa wa mafuta na msukosuko wa kisiasa.

Huyo ni waziri mkuu wa kwanza kuchaguliwa kufuatana na katiba mpya.

Aliyekuwa waziri mkuu, Sushil Koirala, alishindwa na bwana Oli aliyeungwa mkono na familia ya kifalme na watu wa jamii ya Mao miongoni mwa washika dau wengi.

Hata hivyo wachanganuzi wa maswala ya kisiasa wanasema kuwa Bwana Oli atakabiliwa na changamoto ya kuwavutia watu wa jamii ya Madhesi akilinganishwa na waziri mkuu wa zamani bwana Koirala.

Jamii hiyo ya Madhesi inapinga kuakifishwa kwa katiba mpya kutokana na kuwa maswala yao hayajashughulikiwa.

Upinzani wao umepelekea maandamano yalivuruga usafirishaji wa mafuta na bidhaa nyengine muhimu kutoka taifa jirani ya India .