Obama amkejeli rapa Kanye West

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Obama amkejeli rappa Kanye West

Rais wa Marekani Barack Obama ametumia ukumbi wa kukusanya fedha kukejeli nia ya rapa Kanye West kuwania urais 2020.

Obama ambaye yuko San Francisco amemtahadharisha mwanamuziki huyo wa mtindo wa kufoka (Rap) kuwa sharti awatarajie watu wanaoishi maisha yao ni kama wale wasanii wanaoishi maisha yao yote kwenye show ya TV.

Kanye West, alitangaza majuzi tu kuwa atawania urais wa Marekani mwaka wa 2020.

Rais Obama alinukuu ule wimbo wa 'Beautiful Dark Twisted Fantasy' na kumuonya atahadhari dhidi ya kuropokwa tu asije akawaudhi wapiga kura.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption West ametangaza nia ya kuwania uchaguzi wa urais 2020

Obama alimuonya kuwa heri ateleze aanguke lakini asiteleze ulimi kama wabunge kadhaa wa bunge la Congress la Marekani ambao wamepoteza nyadhifa zao baada ya kuteleza ulimi.

''Sharti uwe tayari kukabiliana na watu wenye kuishi maisha yao kama wasanii kwenye shoo za moja kwa moja,''alisema Obama.

Hata hivyo wachanganuzi wa masuala ya kisiasa wanashuku kuwa ujumbe huo wa Obama haukumlenga rapa Kanye West ila mwaniaji kiti cha urais wa chama cha Republican Donald Trump.