Mpalestina mja mzito auawa na jeshi la Israeli

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mwanamke Mpalestina akiomboleza kifo cha jamaa wake kufuatia mashambulizi ya ndege za Israeli

Wizara ya afya huko Gaza inasema mwanamke mmoja Mpalestina aliyekuwa mjamzito, na mwanawe wameuawa katika shambulio lililofanywa na majeshi ya Israel huko .

Maafisa hao wanasema nyumba ya mama huyo iliporomoka baada ya ndege za kijeshi za israeli kufyatua makombora katika majumba yanayoaminika kuwa handaki za wapiganaji wa Hamas.

Mama huyo na mwanawe walishindwa kujinasua nyumba yao ilipoporomoka kutokana na kishindo hicho cha makombora mazito na hivyo kupoteza maisha yao.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Wanne wao wamejeruhiwa.

Nyumba yao inasemekana kuwa mkabala na chuo cha kijeshi cha wanamgambo wa Hamas.

Ndege za kijeshi za Israeli zimeanza upya mashambulio huko Gaza huku kukiwa na wasiwasi wa hali hiyo ya makabiliano huenda ikazidi baina ya waisraeli na wa- Palestina .

Israeli inadai kuwa inalenga vituo vya silaha vya Hamas baada ya roketi mbili kurushwa huko Israel siku 2 zilizopita.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Israeli inadai kuwa inalenga vituo vya silaha vya Hamas

Hofu imetanda kwa mlipuko mpya wa mapigano husan baada ya waziri mkuu wa Israel Benjamini Netanyahu, kutoa amri askari wote wa akiba warejee kazini ilikuimarisha usalama katika mji wa Jerusalem unaotokota kwa uhasama baina ya wapalestistina na wayahudi.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Waziri mkuu wa Israel Benjamini Netanyahu, ametoa amri askari wote wa akiba warejee kazini ilikuimarisha usalama katika mji wa Jerusalem

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani , John Kerry, amezunguzma na waziri mkuu wa Israel Benjamini Netanyahu na vile vile rais wa Palestinian Mahmoud Abbas kujaribu kuidhibiti hali hiyo.