Tanzania: Waziri wa Viwanda na Biashara aaga dunia

Image caption Aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara nchini Tanzania, Dk.Abdallah Kigoda

Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Abdallah Kigoda alifariki dunia siku ya Jumatatu nchini India alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Katibu wa Bunge la Tanzania Dkt Thomas Kashilila amethibitisha taarifa hizo, na kusema kuwa Dkt Kigoda alikuwa akitibiwa katika hospitali ya Apollo, New Delhi nchini India

Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha Ofisi ya Bunge, kimesema taarifa zaidi kuhusu msiba na taratibu za kurejesha mwili nchini Tanzania zitaendelea kutolewa na Serikali na Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia ya marehemu kadiri zinavyoendelea kupatikana