FiFa:Mwana mfalme ataka uchaguzi uharakishwe

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mgombea wa urais katika shirikisho la soka duniani Fifa mwana mfalme Ali Bin al-Hussein anasema kuwa kucheleweshwa kokote kwa uchaguzi wa kumteua mrithi wa Sepp Blatter kutaliyumbisha shirikisho hilo zaidi. Raia huyo wa Jordan anataka kumrithi Blatter aliyesimamishwa kwa mda katika uchaguzi wa mwezi Februari. Lakini Blatter mwenye umri wa miaka 79 pamoja na rais wa UEFA Michel Platini walisimamishwa kazi kwa mda huku FIFA ikitarajiwa kujadiliana kuhusu kuahirisha uchaguzi huo. Ali amesema kuwa hatua hiyo itatoa funzo kote duniani. Ali Bin al-Hussein

Mgombea wa urais katika shirikisho la soka duniani Fifa mwana mfalme Ali Bin al-Hussein anasema kuwa kucheleweshwa kokote kwa uchaguzi wa kumteua mrithi wa Sepp Blatter kutaliyumbisha shirikisho hilo zaidi.

Raia huyo wa Jordan anataka kumrithi Blatter aliyesimamishwa kwa mda katika uchaguzi wa mwezi Februari.

Lakini Blatter mwenye umri wa miaka 79 pamoja na rais wa UEFA Michel Platini walisimamishwa kazi kwa mda huku FIFA ikitarajiwa kujadiliana kuhusu kuahirisha uchaguzi huo.

Ali amesema kuwa hatua hiyo itatoa funzo kote duniani.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Ali Bin Hussein ameketi chini Kushoto

Blatter na Platini wote wameenda mahakamani kupinga kusimaishwa kwazi kwa siku 90.

Katibu mkuu Jerome Valcke pia amesimamishwa kazi.Wote watatu wamekana kufanya uovu.