Marekani:Jeshi la Iraq lichukue Ramadi

Haki miliki ya picha b
Image caption Ramadi

Pentagon imesema kuwa, muda umewadia kwa kikosi cha wanajeshi wa Iraq waliofunzwa na Marekani kuchukua udhibiti wa mji wa Ramadi kutoka mikononi mwa kundi hatari la Islamic State.

Msemaji wa Pentagon kanali Steve Warren amesema kwamba, mashambulio 52 ya angani dhidi ya ngome ya IS katika siku kumi zilizopita yameandaa kikosi hicho kufikia hatua ya mwisho ya kuutwaa mji huo.

Haki miliki ya picha b
Image caption Wanajeshi wa Iraq

Kanali Warren anasema kuwa yatakuwa mapigano makali.