Riek Machar: Sijui nitarudi lini uongozini

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Riek Machar

Makamu wa rais wa zamani wa Sudan Kusini, Riek Machar, anasema kuwa hajui ni lini atarejea nchini humo na kuendelea na kazi yake.

Chini ya muafaka wa amani uliotiwa saini mwezi Agosti, Bw Machar anatarajiwa kurejea nchini Sudan Kusini mwezi ujao ili kufanya kazi kwa pamoja na Rais Salva Kiir ndani ya serikali ya mseto.

Lakini Bwana Machar anasema kwamba kurejea kwake kunategemea hakikisho la usalama.

Anasema sio lazima amuamini Rais Salva Kiir, ili kufanya kazi naye, lakini akaongeza kuwa uamuzi wa hivi majuzi wa kubadilisha mipaka ya taifa hilo unakiuka makubaliano ya amani.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Viongozi wa Sudan Kusini Salva Kiir na aliyekuwa makamu wake Riek Machar wakibadilishana mkataba wa makubaliano ya amani.

Alikosana na Rais Salva Kiir muda mfupi baada ya nchi hiyo kupata uhuru mnamo mwaka wa 2011.

Mapigano ya wenyewe kwa wenyewe yalianza na Bw Machar akaukimbia mji mkuu Juba, mwezi Desemba ya mwaka huo.