Twitter kuwafuta kazi watu 336

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mtandao wa Twitter

Mtandao wa Twitter umesema kuwa unapunguza kazi 336 ikiwa ni asilimia 8 ya ajira zote duniani za mtandao huo kama mpango wa kuimarisha biashara yake.

Upunguzaji huo utaigharimu kampuni hiyo kati ya dola milioni 10 na dola milioni 20 za malipo huku uimarishaji huo ukiigharimu dola milioni 5 hadi 15.

Hisa za twitter zilipanda katika soko lake kufuatia tangazo hilo.

Hatua hiyo inajiri siku chache tu baada ya mwanzilishi mwenza Jack Dorsey kuthibitishwa kuwa meneja mkuu wa kudumu katika kampuni hiyo.

Alikuwa amehudumu kama kaimu meneja mkuu wa kampuni hiyo kwa miezi mitatu baada ya Dick Costolo kujiuzulu mnamo tarehe moja mwezi Julai.

Bwana Costolo ,ambaye amekuwa akiingoza kampuni hiyo tangu mwaka 2010 hadi mwaka huu,amekuwa akipata msukumo kutoka kwa wawekezaji ambao hawafurahii na ukuaji wake.

Katika barua kwa wafanyikazi wa Twitter,Bwana Dorsey aliandika:Tumechukua hatua ngumu zaidi,tunapanga kuwaachisha kazi watu 336 katika kampuni hii.