Upinzani wapinga matokeo ya uchaguzi Guinea

Image caption Cellou Diallo

Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Guinea amejiondoa katika uchaguzi uliofanyika nchini humo akisema kuwa kulikuwa na udanganyifu mkubwa uliotekelezwa na serikali kulingana na kiongozi wake wa kampeni.

Uamuzi huo wa Cellou Diallo wa kujiondoa unajiri wakati ambapo matokeo yanaonyesha kwamba rais Alpha Conde anaongoza kwa wingi wa kura akitafuta kushinda awamu ya pili ya miaka mitano.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wachunguzi wa muungano wa ulaya EU

Wachunguzi kutoka muungano wa Ulaya wanasema kuwa uchaguzi huo ulikuwa wa haki licha ya matatizo makubwa ya vifaa.

Matokeo kamili ya uchaguzi huo yanatarajiwa mwishoni mwa wiki hii.