Uchaguzi wa Handeni mjini waahirishwa TZ

Image caption Tume ya uchaguzi

Uchaguzi wa ubunge katika jimbo la Handeni mjini nchini Tanzania umeahirishwa kufuatia kifo cha mgombea wa eneo hilo kupitia tiketi ya chama cha CCM Daktari Abdallah O Kigoda.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa tume ya Uchaguzi Kailima Kombwey shughuli za kampeni za uchaguzi tayari zimesitishwa katika eneo hilo.

Kombwey amesema kuwa tume hiyo itatangaza ratiba ya tarehe ya uteuzi wa mgombea mwengine kutoka chama cha Mapinduzi CCM.

Hatahivyo kampeni nyingine za Urais na Udiwani katika jimbo hilo zitaendelea kama kawaida.