Kijana aliyevuma kutokana na saa akutana na Bashir

Ahmed Haki miliki ya picha AFP
Image caption Rais wa Marekani Barack Obama na mwanzilishi wa Facebook Mark Zuckerberg walimtetea Mohamed

Mvulana wa umri wa miaka 14 nchini Marekani, aliyegonga vichwa vya habari baada ya kukamatwa kwa kupeleka saa ya kujitengenezea shuleni, amekutana na Rais wa Sudan Omar al-Bashir.

Ahmed Mohamed na familia yake walilakiwa katika ikulu ya rais katika mji mkuu wa Sudan, Khartoum Jumatano, kwa mujibu wa kituo cha redio cha serikali.

Mvulana huyo alifurushwa darasani na kutiwa pingu baada ya mwalimu wake kudhani saa hiyo ilikuwa bomu.

Kukamatwa kwake kulishutumiwa sana. Polisi hawakumfungulia mashtaka yoyote.

Babake mvulana huyo, Mohamed Hassan al-Sufi, ni mhamiaji kutoka Sudan anayeishi Marekani.

Wakati mmoja aliwania urais dhidi ya Bw Bashir.