Mwanamke anayedaiwa kuuza mtoto mtandaoni ashtakiwa

Afrika Kusini
Image caption Mwanamke huyo alikamatwa na kachero aliyejifanya mnunuzi

Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 20 nchini Afrika Kusini amefikishwa mahakamani leo kwa shutuma za kumuuza mwanawe kwa dola 400 kwenye mtandao unaonadi bidhaa wa Gumtree.

Ameshtakiwa kwa kufanya biashara haramu ya binadamu Katika mahakama ya jimbo la KwaZulu-Natal.

Polisi wanasema kuwa mwanamke huyo alitiwa nguvuni Jumanne wiki hii baada ya afisa wa polisi aliyekuwa akifanya upelelezi kujifanya mnunuzi wa mtoto huyo.

Mwanamke huyo hakutakiwa kujibu mashtaka aliposomewa mashtaka hayo katika mahakama Pietermaritzburg.

Hakimu aliagiza azuiliwe hadi Oktoba 26 kesi itakapoendelea tena.

Haki miliki ya picha Gumtree
Image caption Baada ya tangazo la kwanza kufutwa, mwanamke huyo aliweka jingine akidai anauza kiti cha gari cha mtoto

Mtoto huyo wa umri wa miezi 19 amekabidhiwa watu wa kuwatunza watoto.

Mtandao wa Gumtree umekuwa ukishirikiana na wachunguzi.